25 Aprili 2025 - 22:50
Source: Parstoday
Shoigu: Russia inaweza kutumia silaha za nyuklia kukabiliana na mashambulio ya Magharibi

Katibu wa Baraza la Usalama la Russia Sergei Shoigu amesema, Moscow ina haki ya kutumia silaha za nyuklia katika kukabiliana na mashambulio ya nchi za Magharibi.

Shoigu ameyasema hayo katika mahojiano na shirika la habari la TASS na kubainisha kwamba marekebisho yaliyofanywa mwaka uliopita kuhusu mwongozo wa nyuklia wa Russia yanaruhusu kutumia silaha za nyuklia endapo yatafanyika mashambulizi dhidi ya Russia na Belarus.

Katibu wa Baraza la Usalama la Russia amesema: "kuna kampeni ya dhahir shahir inayoendeshwa na Ulaya ya kujiandaa kukabiliana kijeshi na Russia. Jedwali tofauti zinatangazwa za wakati wa kujiri makabiliano hayo kuanzia miaka mitatu hadi mitano. Majeshi na wanasiasa wa Ulaya wanataka wawe wameshajiandaa kwa vita na sisi ifikapo 2030".

Shoigu ameongezea kwa kusema, viongozi wa Ukraine wanafanya juu chini ili kuendeleza uhasama; na mkabala wa kupokea pesa na silaha "waiuzie Ulaya kwa bei ya juu maliasili, eneo la nchi na mustakabali wa watu wa Ukraine", lakini uwezo wao wa kijeshi na kiuchumi ungali dhaifu.

Katibu wa Baraza la Usalama la Russia amebainisha kuwa, uchumi wa Ukraine uko katika hali mbaya sana na unategemea misaada ya Magharibi, huku deni la serikali ya Kiev likiendelea kuongezeka.

Kuhusu juhudi za kuboresha uhusiano kati ya Moscow na Washington, Shoigu pia amesema, serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani imeanza kuchukua hatua kadhaa za kufufua uhusiano wa pande mbili na Russia.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha